1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich yamruhusu Pavard kwenda Inter Milan

30 Agosti 2023

Bayern Munich inatajwa kumuuza Pavard kiasi Euro Milioni 30 kwa Inter Milan

https://p.dw.com/p/4VidK
Fußball Bundesliga | FC Bayern München vs FC Augsburg | Jubel 3:1
Picha: Sven Hoppe/dpa/picture alliance

Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich wameripotiwa kumruhusu mlinzi wake na raia wa Ufaransa Benjamin Pavard kuondoka kwenda Inter Milan ya nchini Italia.

Ripoti za hapa Ujerumani na Italia zimeeleza kwamba Pavard anatarajiwa kusafiri kwa ndege kuelekea nchini Italia kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na kujiunga na Inter Milan ambayo walimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Soma zaidi:  Bundesliga: Manuel Neuer arudi mazoezini

Kwa mujibu wa gazeti la Kiitaliano La Gazzetta dello Sport limeweka wazi kwamba 
Bayern Munich imemuuza mchezaji huyo aliyeshinda Kombe la Dunia 2018 kiasi Euro Milioni 30  pamoja na nyongeza ya Euro milioni 2.

Champions League | Achtelfinale | FC Bayern München - RB Salzburg
Nyota wa Bayern Munich na raia wa Ufaransa Benjamin Pavard akiwan katika hekaheka za mchezoPicha: Matthias Koch/IMAGO

Awali nyota huyo alihusishwa kutakiwa kujiunga na mashetani wekundu Mnchester United kabla ya Inter kuipiga kiwiko United na kuwapa masaa Bayern Munich ya ama kuwauzia Pavard ama watafute mchezaji mwingine.

Soma zaidi:  Kane atamba Bundesliga baada ya kuisaidia Bayern kuifunga Augsburg 3-1

Pavard ambaye bado alikuwa na mkataba wa kuitumikia Bayern hadi 2024 anaelezwa kutokuwa na furaha chini ya Thomas Tuchel na kwamba ameomba kuondoka klabunin humo baada ya miaka minne.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen hapo awali alisema anajiamini
kwamba suluhu inaweza kufikiwa hadi Ijumaa, kabla ya Inter ya Inter kuingilia kati na kuonyesha nia ya kumnasa nyota huyo.

Bayern watahitaji mbadala wake kama walivyofanya pia alimruhusu mlinzi Josip Stanisic kwenda kwa Bayer Leverkusen kwa mkopo.
Trevoh Chalobah wa Chelsea anatajwa kumulikwa na kocha wake wa zamani Thomas Tuchel ambaye kwa sasa ndiye kocha wa Bayern Munich.