1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Chama tawala Msumbiji, Frelimo chamteua kiongozi mpya

6 Mei 2024

Chama tawala nchini Msumbiji cha Frelimo, kimemteua gavana wa mkoa Daniel Chapo kuwa kiongozi mpya.

https://p.dw.com/p/4fXc3
Msumbiji | Uchaguzi wa mitaa | Daniel Chapo
Rais Nyusi amesema kwa uteuzi huo wa mgombea wa urais, Frelimo imepiga hatua muhimu ya kujiandaa kushinda uchaguzi wa Oktoba.Picha: Luciano da Conceição/DW

Uteuzi huo unamfanya Chapo kuwa mrithi wa Rais Filipe Nyusi ikiwa chama hicho kitashinda uchaguzi wa mwaka huu.

Kamati Kuu ya Frelimo ilimteua Chapo aliyekuwa akichuana na wagombea wengine watatu wa ndani, katika hatua ya kushutukiza iliyofuatia siku mbili za mjadala mkali, kuharibika kwa karatasi nyingi za kupigia kura na kujiondoa kwa mshindani wake wa karibu.

Akizungumza usiku wa jana baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu usio wa kawaida wa chama uliofanyika karibu na mji mkuu wa Maputo, Rais Nyusi amesema kwa uteuzi huo wa mgombea wa urais, Frelimo imepiga hatua muhimu ya kujiandaa kushinda uchaguzi wa Oktoba.

Chama hicho kimeshinda kila uchaguzi mkuu tangu kumalizika kwa vita vya kudai uhuru kutoka Ureno mwaka 1975.