1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

EU yakosoa kufungiwa waangalizi wa uchaguzi wa Chad

8 Mei 2024

Umoja wa Ulaya umeikosoa Chad kwa kutowaruhusu karibu waangalizi 3,000 wa uchaguzi kutoka mashirika ya kiraia yaliyofadhiliwa na Umoja huo kuufuatilia uchaguzi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4fcEv
Uchaguzi wa rais Chad
Wapinzani walitoa wito wa kuususia uchaguzi huo, wakiutaja kama uliojaa dosari.Picha: Desire Danga Essigue/REUTERS

Mashirika manne ya kiraia, likiwemo lile la kutetea haki za binadamu la Chad, yameishtumu tume ya uchaguzi iliyoteuliwa na Rais Mahamat Idriss Deby kwa kukataa kuidhinisha wawakilishi wao 2,900 kama waangalizi wa kura.

Soma pia: Kura zaendelea kuhesabiwa baada ya uchaguzi wa rais Chad

Wapinzani wa kiongozi huyo wa kijeshi ambaye naye pia ni mgombea urais walitoa wito wa kuususia uchaguzi huo, wakiutaja kama uliojaa dosari.

Wito wa kuususia uchaguzi ulitolewa baada ya mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kutahadharisha kuwa, uchaguzi wa urais wa Chad hautakuwa huru na haki kutokana na ukandamizwaji wa upinzani.

Jumanne, Jenerali Deby aliupongeza uchaguzi huona kuutaja kama "hatua muhimu ya mageuzi katika kuweka mizizi ya utamaduni wa demokrasia nchini Chad."