1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais Xi wa China akosoa NATO kabla ya ziara yake ya Serbia

7 Mei 2024

Rais wa China Xi Jinping, ameikosoa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kutokana na shambulio lake la "dhahiri" dhidi ya Ubalozi wa China katika nchi ya Yugoslavia mnamo mwaka 1999.

https://p.dw.com/p/4fayn
Xi Jinping ziarani Ulaya
Rais Xi wa China yuko katika ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu kutokee janga Uviko-19.Picha: Ludovic Marin/AP Photo/picture alliance

Rais wa China Xi Jinping, ameikosoa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kutokana na shambulio lake la "dhahiri" dhidi ya Ubalozi wa China katika nchi ya Yugoslavia mnamo mwaka 1999, na ameonya kuwa nchi yake "kamwe haitaruhusu historia ya kutisha kama hiyo kujirudia."

Soma pia: Xi: China ´isichafuliwe jina´ kutokana na mzozo wa Ukraine

Kauli ya Xi ilinukuliwa na gazeti la kila siku la "Serbia Politika" kabla ya kuwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Belgrade, baadaye Jumanne jioni, ikiwa ni kituo kinachofuata katika ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu kutokee janga Uviko-19.

Xi Jinping alianzia ziara yake nchini Ufaransa ambako alikutana na mwenyeji wake Emmanuel Macron na kujadili kuhusu masuala muhimu ya kiuchumi na vita vya Urusi nchini Ukraine. Baadaye Xi ataelekea nchini Hungary.