1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Saudia yakosoa shambulio la Israel kambi ya wakimbizi Gaza

Amina Mjahid
1 Novemba 2023

Saudi Arabia hii leo imekosoa mashambulizi mabaya yaliyofanywa na Israel dhidi ya kambi kubwa ya wakimbizi mjini Gaza na kusababisha mauaji ya watu kadhaa akiwemo kile Israel inachosema ni kamanda wa Hamas.

https://p.dw.com/p/4YH9F
Gaza
Vifaru vya Israel katika mashambulizi ya ardhini huko GazaPicha: Israel Defense Forces/Handout via REUTERS

Saudi Arabia hii leo imekosoa mashambulizi mabaya yaliyofanywa na Israel dhidi ya kambi kubwa ya wakimbizi mjini Gaza na kusababisha mauaji ya watu kadhaa akiwemo kile Israel inachosema ni kamanda wa Hamas.

Kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Saudia, shambulizi hilo limewaua na kuwajeruhi raia wasiokuwa na hatia. Taarifa hii ni ishara ya hivi karibuni inayoonesha kwamba vita kati ya Hamas na Israel vinaanza kutia doa juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya Saudi Arabia na Israel.

Israel imesema ililenga handaki la Hamas katika kambi ya Jabalia na kumuaa kamanda wa kundi hilo Ibrahim Biari, ambaye Israel inaamini alihusika na mashambulizi dhidi yake yaliyofanyika Oktoba 7. Shirika la habari la AFP limesema limeshuduhia miili 47 ikitolewa katika eneo la tukio.