1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yatangaza kumkamata kamanda wa kundi la ADF

Amina Mjahid
20 Mei 2024

Jeshi la Uganda limesema limemkamata kamanda wa kundi la waasi la ADF linaloshirikiana na kundi la dola la kiislamu, ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza mabomu yaliyotumiwa na kundi hilo kutekeleza mashambulizi mabaya.

https://p.dw.com/p/4g4Gw
Beni, DR Kongo | Vikosi vya Uganda na Kongo katika oparesheni ya pamoja
Vikosi vya Uganda na Jmhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa katika oparesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa Kongo.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Kamanda huyo Anywari Al Iraq ambaye ni raia wa Uganda, alikamatwa katika maeneo ya jangwani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kunakopatikana kundi la ADF.

Katika operesheni ya kumsaka kamnda huyo, watu tisa wakiwemo watoto waliokolewa kutoka katika eneo hilo lililopo mkoani Ituri Mashariki mwa DRC, bidhaa nyengine za kutengenezea mabomu pia zilipatikana huko.

Soma pia:Uganda yasema imemkamata kamanda muunda mabomu wa ADF

Kundi hilo la waasi wa ADF lilianza uasi wake nchini Uganda lakini limekuwa na ngome yake nchini Congo,