1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kuanza kuwapeleka wahamiaji Rwanda Julai Mosi

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Serikali ya Uingereza imeiambia Mahakama Kuu mjini London kwamba safari za kwanza za ndege za kuwahamishia waomba hifadhi nchini Rwanda zitaanza kati ya Julai Mosi na Julai 15.

https://p.dw.com/p/4fUv2
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu Rishi Sunak akimpongeza Meya wa Tees Valley Ben Houchen (hayupo pichani) kwa kuchaguliwa tena. Picha: Ian Forsyth/Getty Images

Jaji Martin Chamberlain alifichua tarehe hizo alipokuwa akipanga kusikilizwa kwa pingamizi lijalo la kisheria kwa sheria hiyo mpya ya uhamiaji.

Pingamizi hilo liliwasilishwa na chama cha wafanyakazi wa umma nchini humo. Sheria mpya ya uhamiaji nchini Uingereza inaruhusu mawaziri kupuuza sehemu za sheria za ndani na za kimataifa wakati wa kuamua juu ya uhamishaji huo wa lazima kwa waomba hifadhi.Aprili 22, Waziri Mkuu Rishi Sunak alisema kwamba alitarajia safari za kwanza za ndege kuondoka  ndani ya "wiki 10 hadi 12", lakini hakutoa tarehe kamili.