1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu madhala ya kiutu Gaza

Zainab Aziz
7 Desemba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerelejea ibara ya 99 ya katiba ya Umoja huo ili kulitahadharisha Baraza la Usalama la umoja huo juu ya maafa makubwa yanayoweza kuwakumba binadamu.

https://p.dw.com/p/4ZsLe
USA Generalsekretär der Vereinten Nationen, Antonio Guterres
Picha: Brendan McDermid/REUTERS

Kutumiwa kwa ibara hiyo ni hatua ya nadra. Juu ya hatua hiyo waziri wa mambo ya nje wa Israel Eli Cohen ameukosoa vikali uongozi wa Guterres kwenye Umoja wa Mataifa na amesema unatishia amani ya dunia. Katika kadhia nyingine, Israel imesema itaruhusu kiasi kidogo cha mafuta kuingizwa kwenye Ukanda wa Gaza. Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema nchi hiyo imeidhinisha ongezeko kidogo la mafuta ili kuepusha maafa kwa watu wa Ukanda wa Gaza. Wakati huo huo, askari, vifaru, magari ya kubeba wanajeshi na matingatiga yameingia katika mji wa Khan Younis ambao ni wa pili kwa ukubwa kwenye Ukanda wa Gaza.