1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliokufa katika mafuriko ya nchini Kenya waongezeka

6 Mei 2024

Idadi ya watu waliokufa katika mafuriko ya hivi karibuni nchini Kenya imepanda na kufikia watu 228.

https://p.dw.com/p/4fXbj
Afrika | Mafuriko nchini Kenya
Wataalam wanasema mabadiliko ya Tabia Nchi pia yamezidisha hali ya kujirudia mara kwa mara kwa hali hiyo ya hewa.Picha: IMAGO/Xinhua

Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Mwaura, amesema jana Jumapili kwamba watu 9 walikufa tangu Jumamosi, na zaidi ya watu 200,000 wameathirika na 163,000 wamehamishwa hadi sasa.

Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa masuala ya kibinadamu, mvua za masika zilizoanza kunyesha tangu mwezi Machi zimesababisha mafuriko makubwa katika nchi za Kenya, Tanzania, Burundi, Somalia, Rwanda na maeneo mengine ya Afrika Mashariki.

Mwaka huu hata hivyo, mvua za masika zimekuwa kubwa kutokana na hali ya hewa ya El Nino. Wataalam wanasema mabadiliko ya Tabia Nchi pia yamezidisha hali ya kujirudia mara kwa mara kwa hali hiyo ya hewa.