1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfghanistan

Watu 84 zaidi wapoteza maisha Afghanistan kwa mafuriko

19 Mei 2024

Idadi ya waliokufa kutokana na janga la mafuriko lililoikumba Afghanistan mwishoni wiki hii imefikia watu 84 huku majengo na mali nyingine vikiharibiwa kwa maji.

https://p.dw.com/p/4g3KT
Athari za mafuriko nchini Afghanistan
Athari za mafuriko nchini AfghanistanPicha: AP/picture alliance

Awamu hiyo mpya ya mvua kubwa na mafuriko imeziathiri wilaya nne katika jimbo la Faryab ambapo jana Jumamosi watu 66 walithibitishwa kupoteza maisha, watano wamejeruhiwa na wengine 8 hawajulikani walipo.

Msemaji wa gavana wa jimbo hilo wa kundi la Taliban Esmatullah Moradi amearifu watu wengine 18 walikufa siku ya Ijumaa huku kwa jumla nyumba 1,500 zimeharibiwa kwa mafuriko na mamia ya hekari za mazao zimesombwa.

Idadi hiyo ya vifo inafuatia nyingine iliyotolewa wiki iliyopita na shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP ambayo ilionesha watu 300 wamekufa nchini Afghanistan tangu kuanza kwa msimu wa sasa mvua.

Majimbo ya Ghor na Baghlan ndiyo yameshuhudia uharibifu usio mfano kutokana na mvua hizo.