1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChina

Watu wawili wauawa katika shambulizi la hospitali China

7 Mei 2024

Maafisa nchini China wamesema watu wawili wameuawa na wengine 21 wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa kisu katika hospitali moja kwenye ya kaunti ya Zhenxiong kaskazini-mashariki mwa mkoa wa Yunna

https://p.dw.com/p/4fZsq
Shambulizi la kisu
Watu wawili wameuawa na wengine 21 wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa kisu katika hospitali moja ChinaPicha: McPHOTO/BilderBox/blickwinkel/picture alliance

Mamlaka nchini China zimesema watu wawili wameuawa na wengine 21 wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa kisu katika hospitali moja kwenye ya kaunti ya Zhenxiong kaskazini-mashariki mwa mkoa wa Yunnan.

Mshukiwa ni mwanaume kutoka eneo hilo ambaye aliwavamia wagonjwa na madaktari katika hospitali hiyo bila hata hivyo kutoa sababu zilizopelekea kuchukua hatua hiyo.

Matukio ya ukatili ni nadra mno nchini China, ambako raia hawaruhusiwi kumiliki silaha, lakini katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa kukiripotiwa mfululizo wa mashambulizi ya visu katika maeneo mbalimbali. Haya yanaripotiwa wakati rais wa nchi hiyo Xi Jinping yupo katika ziara yake ya kikazi barani Ulaya. Jana alikutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na baadaye atazitembelea nchi za Hungary na Serbia.