1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Mataifa yakamilishe mkataba wa kudhibiti majanga

Sudi Mnette
4 Mei 2024

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani,Tedros Adhanom Ghebreyesus ameyataka mataifa kuridhia makubaliano ya kusaidia kupambana na miripuko katika siku za usoni, ikiwa ni baada ya athari kubwa za janga la Covid-19.

https://p.dw.com/p/4fUv0
Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya WHO huko Geneva, Uswisi, Aprili 6, 2023.Picha: Lian Yi/Xinhua/picture alliance

Akizungumza mjini Geneva Uswisi amehimiza nchi ambazo hazikukubali kikamilifu kwa maandishi zijiepushe kuzuia maafikiano kati ya Mataifa 194 wanachama wa WHO, ili ulimwengu upate nusura.

Mkataba mpya na mfululizo wa marekebisho ya kisheria katika kushughulika na miripuko unakusudiwa kusaidia ulinzi wa ulimwengu dhidi ya vimelea vipya vya magonjwa ya mripuko baada ya janga la COVID-19 kuua mamilioni ya watu.

Nchi zinatakiwa kukamilisha mazungumzo juu ya makubaliano hayo Mei 10, kwa nia ya kuipitisha katika mkutano wa kila mwaka wa WHO baadae mwezi huu, lakini vyanzo vinavyohusika vinasema bado kuna kuwa tofauti kubwa zilizosalia.