1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zaidi ya watu 4,000 wahamishwa kutoka eneo la Kharkiv

Tatu Karema
12 Mei 2024

Zaidi ya watu 4,000 wamehamishwa kutoka maeneo ya mpakani katika mkoa wa kaskazini-mashariki wa Kharkiv nchini Ukraine kufuatia shambulizi la kushtukiza la Urusi lililoanza siku ya Ijumaa katika eneo hilo

https://p.dw.com/p/4fl0B
Majengo yalioharibiwa na shambulizi la Urusi mjini Kharkiv nchini Ukraine mnamo Mei 10,2024
Majengo yalioharibiwa na shambulizi la Urusi mjini Kharkiv nchini UkrainePicha: Vyacheslav Madiyevskyy/Ukrinform/IMAGO

Katika ujumbe aliochapisha katika mitandao ya kijamii, Synegubov amesema kwa ujumla, watu 4,073 wamehamishwa siku moja baada ya Urusi kuteka vijiji vitano katika eneo hilo.

Zelensky asema vikosi vyake vyakabiliana na uvamizi wa Urusi

Hapo jana, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alisema kuwa vikosi vya nchi yake vimekuwa vikifanya mashambulizi ya kukabiliana na uvamizi huo wa Urusi katika vijiji vya mpakani vya eneo hilo la Kharkiv.

Soma pia:Mamia ya watu wahamishwa kutoka mpaka wa Ukraine

Kwa wiki kadhaa sasa, maafisa wa Ukraine walikuwa wameonya kwamba huenda Urusi ikajaribu kushambulia maeneo ya mpakani ya kaskazini mashariki na kutumia nguvu yake wakati Ukraineikipambana na kucheleweshwa kwa msaada wa mataifa ya Magharibi na pia uhaba wa wapiganaji.