Katika duru ya kwanza ya mashindano ya kombe la Ujerumani-DFB Pokal, Shalke 04 iliichapa jana klabu ya Tenigen mabao 11-1.
Mamlaka za usalama nchini Ukraine zimesema zimebaini njama ya Urusi ya kufanya shambulizi dhidi ya Rais Volodymyr Zelensky na wanasiasa wengine wa nchi hiyo.
Umoja wa Ulaya umetangaza msaada wa dola milioni 125 kuyapiga jeki mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasiyo ya kiserikali yanayowasaidia watu nchini Yemen.
Italia imetangaza marufuku kwa mashirika ya hisani kutumia viwanja vya ndege kwenye visiwa vitatu kurusha ndege ambazo husaidia kutafuta boti za wahamiaji wanaohitaji msaada baharini.