Katika ligi ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga, Schalke iliifunga jana Augsburg mabao 3-1 na Hamburg ikaiadhibu Nürnberg 2-0.
Mabingwa wa Bundesliga Bayer Leverkusen waendeleza rekodi yao ya kutoshindwa, huku zikiwa zimesalia mechi tatu msimu wa ligi kukamilika // Bayern na Dortmund zajiandaa kwa michuano muhimu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwa na msimu usioridhisha katika ligi ya nyumbani //Na utasikia kwa nini ramani iliyochorwa kwenye jezi ilisababisha mechi ya Kombe la SHiriksiho Afrika kufutwa
Ligi Kuu ya Kandanda hapa Ujerumani - Bundesliga inaelekea ukingoni. Baada ya bingwa kujulikana sasa macho yote yamegeuka katika nafasi za kucheza kandanda la Ulaya. Kwa mengi zaidi kuhusu mechi za wikiendi hii Suleman Mwiru amezungumza na Bruce Amani kuhusu michezo ya wikiendi hii na ambao utatangazwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook wa DW Kiswahili na kupitia redio mbalimbali washirika.
Katika michezo, nafasi ya kwanza inamaanisha ubingwa. Mbali na talanta unahitaji washauri na wakufunzi bora watakao kuongoza kufikia ubingwa. Hawa huchangia ushindi nyuma ya pazia na kumsaidia mchezaji kuvikabili vikwazo na ukiritimba unaojitokeza katika safari ya mashindano. #vijanamubashara