Deutsche Welle: Madaktari wa hospitali za umma nchini Kenya wamaliza mgomo wao baada ya serikali kukubaliana nao juu ya kutekeleza matakwa ya madaktari hao.
Kenya na Uganda zimeafikiana kuweka kando tofauti zao na kuimarisha biashara ya mafuta kati ya nchi hizo mbili.
Katika safu yetu ya Msichana Jasiri, mjadala unaopewa nafasi unahusu. "Wasichana katika kuzienzi tamaduni zao."
Zaidi ya asilimia 90 ya shule nchini Kenya zimefunguliwa leo, baada ya kufungwa kwa takribani wiki mbili kutokana na mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu 270.