Katika ligi ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, timu ya Bayern Munich inacheza na FC Cologne leo.
Kutana na wanawake hawa wenye ulemavu waliamua kujiingiza kwenye mchezo wa mpira wa mikono na namna wanavyosakata mchezo huo.
Ujerumani itafungua pazia watakapokipiga na Scotland mnamo Juni 14 katika dimba la Allianz Arena mjini Munich, huku fainali ikitarajiwa kuchezwa Julai 14 katika uwanja wa Olympiastadion mjini Berlin. Sikiliza mahojiano kati ya John Juma na Josephat Charo wa dawati la michezo la DW Kiswahili.
Bingwa mara mbili wa Michezo ya Olimpiki, Caster Semenya, ameomba kufadhili mapambano yake ya kisheria dhidi ya sheria zinazowataka wanariadha wa kike wenye viwango vikubwa vya homoni ya testosteroni kumeza dawa.