Ghasia zimeendelea nchini Ugiriki baada ya mamia ya vijana wanaopinga mipango ya serikali ya kubana matumizi kupambana na polisi.
Yaliyomo katika taarifa ya habari za ulimwengu kwenye matangazo ya Dw Jioni, ni ziara ya rais wa China Xi Jinping barani Ulaya,na Matumaini ya kufikiwa makubaliano kuhusu vita vya Gaza yafifia nchini Misri.Utasikia pia makala ya maoni mbele ya meza ya duara inayojadili athari za mabadiliko ya tabia nchi Afrika Mashariki.
Mamlaka nchini Kenya zimesema kuwa idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko imeongezeka hadi kufikia watu 228.
Wananchi wa Panama wameanza hivi leo kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa urais unaowashirikisha wagombea wanane.