Deutsche Welle: Timu ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Hertha Berlin, yamtema kocha wake, Markus Barbel, aliyekuwa akiifundisha timu hiyo tangu Julai 1 mwaka jana.
Ligi Kuu ya Kandanda hapa Ujerumani - Bundesliga inaelekea ukingoni. Baada ya bingwa kujulikana sasa macho yote yamegeuka katika nafasi za kucheza kandanda la Ulaya. Kwa mengi zaidi kuhusu mechi za wikiendi hii Suleman Mwiru amezungumza na Bruce Amani kuhusu michezo ya wikiendi hii na ambao utatangazwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook wa DW Kiswahili na kupitia redio mbalimbali washirika.
Bayer Leverkusen wameshinda taji la ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga kwa mara ya kwanza katika historia yao ya miaka 120.
Bayer Leverkusen inaendelea kuandikisha rekodi ya ushindi wa tisa mfululizo ya kutopoteza katika michezo 41 ya mashindano yote msimu huu na wanahitaji ushindi mmoja tu kutoka kwa mechi zao zilizosalia ili kushinda taji la Bundesliga kwa mara ya kwanza.