David Beckham amelifikia lengo alilojiwekea alipowasili Los Angelea 2007.Timu anayoiongoza ya L A Galaxy imenyakuwa ubingwa wa ligi kuu ya Marekani.
Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami NATO yameonesha wasiwasi kuhusu mashambulizi yanayohusishwa na Urusi ambayo yanatajwa kuathiri Jamhuri ya Czech, Estonia, Ujerumani, Latvia, Lithuania, Poland, na Uingereza.
Mkuu wa ofisi ya haki ya Umoja wa Mataifa Volker Turk ametoa wito kwa serikali ya Georgia kuondoa mswada wenye utata ulio katika mchakato wa kibunge na kuelezea wasiwasi wake kuhusu ukandamizaji wa polisi kwa umma.
Timu ya Bayer Leverkusen imeonesha kuijongelea fainali ya Ligi ya Europa baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Roma katika mchezo wake wa ugenini huko Italia kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa kwa mechi 47 walizocheza.