DeutscheWelle:Wakenya wanasubiri kwa hamu kubwa kujua kama watuhumiwa sita,wakiwemo wagombea wawili wa kiti cha rais watatakaswa au watahitaji kujibu mashtaka ya ICC.
Mzozo wa ardhi ya Ndabibi katika kaunti ya Nakuru unaendelea kugonga vichwa vya habari ambapo bunge la kitaifa sasa limeelezwa kwamba zaidi ya watu 140,000 wamefurushwa kutoka kwenye makao yao.
Rais William Ruto amewakosoa wabunge kwa kutelekeza agenda yake ya kutoa nafasi za ajira zikiwemo nafasi kwenye mataifa ya nje na badala yake amewataka kuunga mkono ajenda hiyo inayonuia kupunguza tatizo la ajira.
Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia mafuriko na maporomoko ya tope yanayosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini Kenya imefikia 169, huku wengine 200,000 wakiachwa bila makaazi.