Katika ligi kuu ya Hispania, La Liga, Malaga kuvaana na Villareal na katika ligi ya England, Liverpool yailazimisha Machester City suluhu ya 1-1.
Wanamgambo wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wameanza kupanua mamlaka yake ndani ya Yemen na katika kanda nzima Mashariki ya Kati.
Wajerumani wanajivunia miji yao, ambayo aghalabu husifiwa kwa uvumbuzi na kuwa rafiki kwa mazingira. Lakini hilo halijawavimbisha kichwa. Wako Wajerumani wanaovutiwa na kujifunza kuhusu miji mingine duniani inavyotatua changamoto kwa wakaazi wake. Mfano ni mji mkuu wa Rwanda, Kigali. Rachel Nduati alishuhudia hilo hivi karibuni. Tizama video hii.
Zimbabwe imeanza wiki hii kutumia sarafu yake mpya inayofahamika kama ZiG na kuachana na sarafu ya zamani, katika jaribio lake la hivi punde la kutatua mzozo wa kifedha.