1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa asifia mafanikio ya miaka 30 ya ANC madarakani

Bruce Amani
13 Januari 2024

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesifu kile alichokiita hatua muhimu zilizopigwa na chama chake tawala cha African National Congress - ANC wakati chama hicho kikiadhimisha miaka 112 ya kuasisiwa kwake

https://p.dw.com/p/4bCnb
Südafrika Der Präsident des Afrikanischen Nationalkongresses (ANC), Cyril Ramaphosa
Picha: Denis Farrell/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa leo amesifu kile alichokiita hatua muhimu zilizopigwa na chama chake tawala cha African National Congress - ANC kutoka kwenye magofu ya ubaguzi wa rangi miaka 30 iliyopita hadi uchaguzi wa kihistoria unaotarajiwa mwaka huu.

Soma pia: ANC yaadhimisha miaka 112 ya kuasisiwa kwake Afrika Kusini

Ramaphosa, aliyevalia rangi za chama za kijani na njano, aliwahimiza makumi kwa maelfu ya wafuasi wa ANC kulinganisha hali ya leo ya taifa na ile iliyorithiwa na Nelson Mandela katika mwaka wa 1994. Chama hicho kinaadhimisha leo miaka 112 ya kuasisiwa kwake.

Licha ya kukumbwa na uhaba wa fedha na kushambuliwa kuhusiana na rushwa, uchumi dhaifu, kukatika kwa umeme na kuongezeka kwa uhalifu, uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa ANC bado inaonekana kupata ushindi katika uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kati ya Mei na Agosti.