Deutsche Welle: Kwa uchache watu wanane wahofiwa kufariki dunia na wengi zaidi hawajuilikani walipo kufuatia ajali ya boti kwenye kisiwa cha Lamu nchini Kenya.
Watu wasiopungua 188 wamekufa nchini Kenya kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi tangu mwezi Machi, huku wengine karibu 200,000 wakilazimika kuyahama makazi yao.
Idadi ya watu waliokufa katika mafuriko ya hivi karibuni nchini Kenya imepanda na kufikia watu 228.
Rais wa Kenya William Ruto ameahirisha mpango wa kuzifungua tena shule wiki ijayo hadi kutakapotolewa tangazo jingine, wakati mvua kubwa na mafuriko yaliyowaua watu zaidi ya 200 yakiendelea.